Kwa picha: Ijumaa ya pili ya mwezi wa Ramadhani.. malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na pembezoni mwake umekua uwanja wa kiroho na ibada.

Maoni katika picha
Mwezi wa Mwenyezi Mungu umekuja na Baraka, rehma na Maghfira, mwezi bora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na michana yake ni bora zaidi ya michana mingine, usiku wake ni bora kuliko usiku mwingine, saa zake ni bora kuliko saa zingine, mwezi ambao waislamu wameitwa kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anawakirimu… kutokana na utukufu huo, waumini wanahuisha usiku wa Ijumaa ya pili ya mwezi huu mtukufu kwenye malalo mbili tukufu; ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Wamemaliza kumi la kwanza la rehma, wanaingia kumi la pili la maghfirah, uwanja na maeneo yanayo zunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yamekua uwanja wa kiroho na kiibada, pamoja na kuongezeka kwa joto lakini pamejaa waumini waliokuja kutoka ndani na mje ya mkoa wa Karbala, wamekuja kufanya ibada katika eneo hili takatifu.

Mji mtukufu wa Karbala umeshuhudia ongezeko kubwa la mazuwaru kutoka mikoa tofauti walio kuja kufanya ibada za usiku wa Ijumaa ya pili katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, asilimia kubwa wamefika tangu asubuhi kwa ajili ya kuusubiri usiku huu mtukufu.

Watumishi wa malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wanakauli mbiu isemayo (Kumhudumia zaairu aliyefunga ni utukufu kwetu), wanafanya kila wawezalo kuhakikisha mazuwaru wanatekeleza ziara na ibada zao kwa Amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: