Kila siku asubuhi idara ya wahadhiri wa kike inafanya kisomo cha Qur’ani ndani ya mwezi huu wa Ramadhani.

Maoni katika picha
Qur’ani tukufu ni funguo za hazina za ghaibu na za mbinguni pia ndio kilele cha utukufu na ukamilifu wa kila jambo, ni mwongozo wa watu wote katika kila zama, kama anavyo sema Mwenyezi Mungu mtukufu: (Hakika hii Qur’ani inaongoa kwenye yaliyo nyooka kabisa..), mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Qur’ani, Mwenyezi Mungu aliutukuza kwa kuishusha katika mwezi huo, nayo imebainisha kila kitu, kwa ajili ya kunufaika na utukufu wa mwezi huu, Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya harakati mbalimbali za Qur’ani, idara ya wahadhiri wa kike inaratiba maalumu ya usomaji wa Qur’ani yenye vipengele tofauti.

Makamo kiongozi wa idara ya wahadhiri wa kike Ustadhat Taghridi Abdulkhaaliq Tamimiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kila siku tunafanya kikao cha usomaji wa Qur’ani katika sardabu ya Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kisomo hiki kitaendelea mwezi mzima wa Ramadhani, katika usomaji kuna vitu vingi, miongoni mwa vitu hivyo ni:

  • - Kusoma juzuu moja la Qur’ani kila siku.
  • - Kufafanua maana za baadhi za aya zilizo somwa katika juzuu husika.
  • - Kutoa ufafanuzi kuhusu hadithi zinazo zungumzia tabia njema za kiislamu kutoka kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), na zenye kufungamana na aya zilizo somwa katika juzuu husika.
  • - Kusoma visa na mafunzo yanayo patikana katika matukio ya kihistoria yaliyo tokea ndani ya mwezi wa Ramadhani na kutajwa katika Qur’ani tukufu.
  • - Kuadhimisha yaliyo tokea katika mwezi wa Ramadhani.
  • - Kuhuisha siku za Lailatul Qadri.
  • - Kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s) na kuomboleza kifo cha baba yake (a.s)”.

Akabainisha kua: “Katika ratiba hii wanashiriki wanafunzi waliosoma katika kozi mbalimbali zilizo tolewa na idara hii pamoja na mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), kisomo huanza saa nne hadi saa sita asubuhi kila siku”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: