Baada ya kufanikiwa katika onyesho lake la kwanza: Filam ya (Rozaba) yaonyeshwa katika mji wa Bagdad na Basra.

Maoni katika picha
Baada ya mafanikio na mwitikio mkubwa iliyo pata filam ya (Rozaba) inayo elezea kisa cha swahaba mtukufu Salmani Muhammadiy (r.a) katika ukumbi wa kitaifa wa maigizo kwenye mji mkuu Bagdad, sasa inaonyeshwa katika mkoa wa Basra kwenye ukumbi mkuu wa snema, kuanzia siku ya (10 Ramadhani 1440h) na kuendelea hadi siku za Iddi tukufu saa tatu na nusu jioni.

Itaonyeshwa tena katika uwanja wa michezo wa taifa kuanzia Jumamosi (12 Ramadhani 1440h) sawa na (18 Mei 2019m) saa tatu na nusu jioni.

Kumbuka kua filam ya (Rozaba) inaeleza kisa cha swahaba mtukufu Salmani Muhammadiy (r.a), kuanzia utoto wake pamoja na hatua mbalimbali alizopitia katika maisha yake hadi alipo ingia katika Dini ya kiislamu, Imetengenezwa na kituo cha Alkafeel cha Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya usimamizi wa Ustadh Azhar Khamisi Ahmadi na jopo wa watumishi wa kituo hicho.

Picha za filamu zimepigwa katika miji mikubwa ya uigizaji wa snema jamhuri ya kiislamu ya Iran, ambayo ni miji ya Nuru Tabaan, iliyo anzishwa na jopo la wataalamu wa kitaliano walio bobea katika utengenezaji wa filam, wakati wa kutengeneza filam ya (Muhammad Rasulu Llah), filamu hii ina dakika (59), kazi ya kupiga picha ilichukua siku (24), kazi hiyo ilikamilika mwishoni mwa mwaka uliopita 2018m.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: