Maelekezo muhimu ya Marjaa Dini mkuu kwa vijana wa Iraq.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ametoa maelekezo kadhaa kwa vijana wa Iraq, kupitia mimbari ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa Imamu Hussein (a.s) leo (11 Ramadhani 1440h) sawa na (17 Mei 2019m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), khutuba ilikua na usia mwingi kwa vijana pamoja na kueleza mazingira halisi tunayo ishi kwa sasa, miongoni mwa yaliyo husiwa ni:

  • - Hakika vijana ndio mustakbali wa kila taifa.
  • - Kila taifa linalotaka maendelea hutegemea vijana.
  • - Baadhi ya vijana wa leo wanachamgamoto nyingi.
  • - Vijana wanapopata changamoto wanahitaji mtu wa kuwaongoza.
  • - Tunapo mkosa kijana mmoja tunakua tumepata hasara kama jamii kwani angeweza kutengeneza mamo mengi na tukipoteza wawili, hasara inakua kubwa zaidi na wakiwa watatu hasara ni kubwa mno… na kuendelea.
  • - Asilimia kubwa ya vijana wa leo wanawajibika na wanajua mambo.
  • - Mnatakiwa kufanya kazi kwa bidii umri wa ujana ndio wenye nguvu za kiakili na kimwili.
  • - Tumieni wakati vizuri.
  • - Taifa hujengwa kwa kufanya kazi kwa bidii na ikhlasi (uaminifu).
  • - Jifunzeni kufanya jitihada katika maisha yenu.
  • - Lazima uwe na malengo na ufanye kazi kutokana na malengo yako.
  • - Lazima uwe na mkakati wa kutekeleza malengo yako.
  • - Haifai kumaliza muda kwa kufanya starehe na mambo ya kipuuzi.
  • - Wangapi wamemaliza ujana wao kwa mambo ya kipuuzi na sasa wanajuta.
  • - Wangapi walifanya mambo ya hovyo katika ujana wao bado athari za upuuzi wao zinawaandama hadi sasa.
  • - Wangapi wanajuta kwa kupoteza ujana wao.
  • - Haitakiwi kujaribu kila kitu, baadhi ya vitu ukivijaribu unaanguka.
  • - Ewe kijana unatakiwa kuomba ushauri na kujifunza kwa wakubwa na ufanyie kazi nasaha zao.
  • - Ewe kijana usidanganyike na ujana ukajiona unajua kila kitu na unaweza kila kitu.
  • - Mzee alikua kijana, anajua mazingira ya ujana. Anapo kupa nasaha anakuambia mambo anayojua.
  • - Vijana wangapi leo wanamaliza muda wao kwa mambo yasiyokua na faida??.
  • - Tunapo ona baadhi ya vijana wanatumia muda wao kwa mambo yasiyokua na faida tunaumia sana kwa sababu tunafahamu mambo hayo yatawafikisha wapi.
  • - Vijana fikirieni mustakbali wenu, miongoni mwa sababu za kutofanikiwa ni kuangalia miguuni kwako, yaani kuto angalia mbele.
  • - Mtu anaangalia leo yake tu, weka malengo ya mustakbali wako na utembee kufuata malengo hayo unaweza kufanikisha malengo yote au hata theluthi yake.
  • - Vijana mnatakiwa kutafakari na kuweka mikakati.
  • - Chukueni nasaha kutoka kwa watu wenye manufaa nanyi.
  • - Kuna wanaotaka kuweka sumu katika asali na kupanda juu ya mabega ya vijana kwa faida zao binafsi.
  • - Hamna haki ya kuwatumia vijana kama daraja la kufikia mambo yenu.
  • - Naziomba sana familia zikae na vijana wao ziwashike mikono na kuwaongoza.
  • - Kaeni nao na muwatahadharishe mambo mabaya kwao, msiwaache peke yao wakafanya watakavyo.
  • - Starehe ya duniani na akhera ni kukaa na watoto wako na wao kusikia maelekezo yako.
  • - Jambo hili limeanza kupotea.
  • - Maumbile ya kibinaadamu yanamtaka mzazi akae na watoto wake, na mtoto anapenda kusikiliza mafundisho kutoka kwa wazazi wake.
  • - Enyi vijana mnatakiwa mfuate watu wakukupeni ushauri bora wenye hekima na busara.
  • - Enyi vijana someni, elimu huanzwa wala haimalizwi.
  • - Enyi vijana fanyieni kazi nasaha, wekeni malengo na mikakati kwa ajili ya mustakbali wenu mkiyafanya hayo kwa umakini bila shaka mtafaulu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: