Maoni katika picha
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano Mhandisi Hassan Hilliy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu maonyesho haya kua: “Maonyesho yamesimamiwa na mzee wa wapiga picha wa Hilla Imaad Mustwafa, nayo ni matokeo ya kamera ya mzazi wake aliyekua mmoja wa wapiga picha muhimu katika zama zake, aliweza kutengeneza picha kadhaa za viongozi, wanachuoni, mazingira na mengineyo yaliyo kuwepo katika mji wa hilla, sambamba na malalo pamoja na maqamu zilizopo katika mkoa huu, picha hizi zinatokana na juhudi za mzazi wake, kwani alitaka kuonyesha mambo yaliyopo katika mji huu kwa kutumia picha”.
Akasema kua: “Pamoja na udogo wa maonesho haya lakini yamebeba historia ya mji wa Hilla ya miongo kadhaa, tunatarajia kupanua maonyesho haya siku za mbele kwa msaada wa Ataba mbili tukufu, ukizingatia kua picha nyingi za mtaalamu huyu zinatakiwa kutangazwa”.
Kumbuka kua hili ni miongoni mwa makongamano makubwa ya kidini na hufanywa kila mwaka katika kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s), linalenga kuonyesha nafasi ya pekee aliyokua nayo Imamu (a.s), na kuonyesha msimamo wake dhidi ya kiongozi wa zama zake ambaye ni Muawiya, na kuangazia changamoto na mitihani aliyo pata Imamu (a.s) katika maisha yake.