Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika maonyesho ya maarifa ya Qur’ani ya kimataifa awamu ya (27) kupitia kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, yanayo simamiwa na wizara ya utamatuni na maelekezo ya Iran katika mji mkuu wa Teheran chini ya kauli mbiu isemayo: (Qur’ani ndio maana ya uhai) katika muswala wa Imamu Khomeini, yataendelea hadi (24 Mei 2019m) jumla ya taasisi (300) zinashiriki kutoka katika nchi (18).
Kama kawaida yake katika maonyesho ya kitaifa na kimataifa, wasimamizi wa tawi hili hufanya kila wawezalo ili kupata mafanikio mazuri yanayo endana na utukufu wa Ataba, tawi lina makumi ya vitabu na machapisho ya Qur’ani pamoja na majarida mbalimbali yaliyo chapishwa na kitengo hicho pamoja na vituo vilivyo chini yake katika mikoa ya Iraq, wanakila kitu kinacho weza kuchangia ubora kwenye sekta ya vitabu vya kitafiti, kidini na mambo ya turathi.
Tawi limepata mwitikio mkubwa tangu siku ya kwanza ya ufunguzi wa maonyesho haya, limetembelewa na makamo waziri wa utamaduni wa Iran katika mambo ya Qur’ani na Itra, rais wa maonyesho haya Abdul-Haadi Fiqhiy Zaada, waziri wa utamaduni na maelekezo wa Iran Dokta Abbasi Swalehe, raisi wa askari wa Iran Sardaar Hashtari pamoja na viongozi wengine, wote wamesifu ushiriki wa Atabatu Abbasiyya kupitia kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha wahi kushiriki katika maonyesho haya, imekua ikifanya vizuri katika ushiriki wake na kufanikiwa kupata zawadi katika kila ushiriki kutokana na mpangilio, kukubalika na utendaji.