Msaada wa kimkakati kwa wapiganaji wa Hashdi Shaábi na ugawaji wa chakula kwa familia za mashahidi katika mkoa wa Baabil.

Maoni katika picha
Idara ya mkoa wa Baabil chini ya ofisi ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu, sawa na idara zingine zinazo fungamana na Ataba katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, wanafanya kazi ndani na nje ya mkoa wa Baabil, ya kusaidia wapiganaji wa Hashdi Shaábi katika mji wa Mosul.

Kiongozi wa idara bwana Swadiq Ubaidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kazi za idara zinaendelea katika mwezi wa Ramadhani na hata katika miezi mingine, lakini katika mwezi huu tunazifanya kwa wingi tena katika sekta zote, katika sekta ya huduma za kibinaadamu hua tunaendelea kugawa chakula kwa familia hizi, tunagawa chakula mwezi mzima wa Ramadhani”.

Ubaidi akaongeza kua: “Sehemu ya pili ya kazi zetu ni kutoa msaada kwa wapiganaji wa Hashdi Shaábi kikosi cha 44/ katika mji wa Mosul na Hadhar, jukumu hilo limetekelezwa na (Msafara wa 15 Shabani), nao ni katika misafara ya idara hii na uliwasaidia wapiganaji kwenye vita ya ukombo wa Iraq dhidi ya magaidi wa Daesh”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: