Kuvishwa taji kikundi cha Najafu kwa ushindi wao: Kumekamilisha awamu ya tano ya mashindano ya Quráni ya vikundi ya kitaifa.

Maoni katika picha
Katika ukumbi mtakasifu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) jioni za mwezi mtukufu wa Ramadhani, ya jana Jumamosi (12 Ramadhani 1440h) sawa na (18 Mei 2019m) imekamilika awamu ya tano ya mashindano ya Quráni ya vikundi, yanayo simamiwa na kituo cha miradi ya Quráni katika Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kufuzu kikundi cha Najafu baada ya mchuano mkali kati yake na kikundi cha Karbala kilichoibuka mshindi wa pili.

Hafla ya ufungaji imehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar na jopo la wajumbe wa kamati kuu pamoja na maraisi wa vitengo sambamba na kundi la mazuwaru na washirika wa vikundi vilivyo shiriki katika mashindano.

Jopo la majaji lilikua na Dokta Munidi Kaabi, na msomaji Ammaari Kinani, na haafidhu wa Quráni Sayyid Mahadi Wardi, mashindano yalianza tangu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, yalikua na mchuano mkali katika hatua zote, na hatimae vikundi vifuatavyo vikashinda kama ifuatavyo:

Washindi wa kwanza: kikundi cha Najafu Ashrafu kilichokua na: (Msomaji Muhammad Saidi, Haafidhu Fahadi Haadi, Mfasiri Ahmadi Nasru-Dini)

Washindi wa pili: kikundi cha Karbala tukufu kilichokua na: (Haafidhu Hamidi Takfifu, Mfasiri Hamza Daakhil, Msomaji Sajjaad Hussein).

Washindi wa tatu: kikundhi cha mkoa wa Bagdad kilichokua na: (Msomaji Ali Jawaad, Haafidh Hussein Muhammad Shalaal, Mfasiri Nizaar Aáraji).

Washindi wa nne: kikundi cha mkoa wa Waasit kilichokua na (Msomaji Ali Qaaid, Haafidhu Ali Fariji na Mfasiri Fuadi Fadhili).

Kumbuka kua zawadi ya mshindi wa kwanza wa maonyesho haya ni bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s), ambao watakaa nayo mwaka mzima, na kwenda Umra, amma kikundi cha Karbala tukufu kilicho pata nafasi ya pili, kimepewa midani ya fedha, wakifatiwa na kikundi cha Bagdad kilicho shinda nafasi ya tatu na kikapata midani ya silva, vikundi vyote vilivyo shiriki katika mashindano haya pia vimepiwa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: