Baina ya haram mbili tukufu: wafungaji wanapewa juisi kila siku.

Maoni katika picha
(Mfungaji anafuraha mbili, wakati wa kufturu na siku atakayo kutana na Mpla wake) ni ubora ulioje kuja kufturu jirani na malalo mawili matakatifu la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na hilo kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu ambacho kipo chini ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya kimeamua kushirikiana na waliofunga waliopo katika eneo hilo kwenye furaha ya kufturu, kwa kugawa kiasi kikubwa cha juisi ya baridi karibu na adhana ya Magharibaini kwa ajili ya kujiandaa na futari.

Mazuwaru wanakuja kutoka maeneo mbalimbali wanafurika katika eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukuku, husimama kwa mistari ili waweze kupata tabaruku kutoka kwa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), hukusanyika sehemu zinapotolewa juisi za baridi na watumishi wa Ataba mbili tukufu saa moja kabla ya muda wa kufturu, viwango vya joto vinaendelea kuongezeka kwa sababu ya kuingia kipindi cha kiangazi, kwa hiyo vinywaji vya baridi husaidia sana kupoza kuu zao baada ya kufturu.

Kuna aina mbalimbali ya juisi wanazo pewa walio funga, kuna juisi ya ukwaju, rehani na zafarani, pamoja na aina zingine nyingi zinazo saidia kukata kiu ya aliye funga.

Kumbuka kua kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu chini ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya sawa na vitengo vingine vya Ataba, kinafanya kazi kubwa na kutoa huduma mbalimbali kwa zaairu wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: