Mtandao wa kimataifa Alkafeel unatoa wito kwa wapenzi na wafuasi wote wa Ahlulbait (a.s) mashariki na magharibi wanaopenda kumzuru mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa niaba, kwenye kumbukumbu ya kuzaliwa kwake katika kaburi lake takatifu huko Jannatul-Baqii, wajisajili katika ukurasa wa ziara kwa niaba.
Ibada ya ziara ni miongoni mwa huduma zinazo tolewa na mtandao wa Alkafeel kupitia idara ya matangazo ya kimtandao katika mwezi wa Ramadhani, ambapo inajumuisha ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na usomaji wa dua ya Iftitaahi na ziara ya Imamu Ali (a.s) katika usiku wa kifo chako pamoja na ziara mahasusi katika siku za Lailatul Qadri na usiku wa Iddul-Fitri pamoja na mchana wake.
Idara imeandaa watu watakao fanya ibada hizo kwa niaba ya kila atakaesajili jina lake katika ukurasa wa ziara kwa niaba: (http://alkafeel.net/zyara).