Kwa picha: Mapambo na mauwa ya asili yalipamba dirisha la Abulfadhil Abbasi katika usiku wa kuzaliwa kwa kaka yake mkubwa.

Maoni katika picha
Kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) limewekwa makumi ya mapambo na mauwa, kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s).

Ustadh Zainul-Aabidina Adnani kutoka idara ya uangalizi wa haram na kiongozi wa kupamba haram takatifu amesema kua: “Maua haya yametolewa na waumini wanaoguswa na tukio la kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Akaongeza kua: (Idadi ya mitungi ya mauwa iliyo wekwa juu ya kaburi tukufu imefika (40) arubaini, ikiwa na makumi ya mauwa asilia ya aina tofauti, harufu ya mauwa hayo inasikika hadi katika maeneo mengine ya haram tukufu”.

Kumbuka kua mauwa ya asili ambayo huwekwa katika ukumbi wa haram katika maadhimisho tofauti, hufuata viwango vilivyo wekwa na Ataba tukufu, maeneo ya nje yanayo zunguka haram pamoja na barabara kuu zinazo elekea katika haram zimewekwa mapambo mbalimbali kama ishara ya kujiandaa kusherehekea kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: