Ni jambo la kuwaida waumini kukutana na kuonyesha furaha zao kwa kuzaliwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) ndani ya mwezi wenye baraka kubwa mwezi wa Mwenyezi Mungu, ametakasika Mola mtukufu aliye tuliza macho ya walii wake kwa kumtunuku mtoto katikati ya mwezi wa baraka, hakika umekutana utukufu wa tukio na utukufu wa kipindi, haya ni mazingira magumu kuelezewa na mtu wa kawaida, ni maamuzi ya Mwenyezi Mungu muumbaji wa kila kitu.
Kutokana na kumbukumbu hii na umuhimu wa kuadhimisha alama za Mwenyezi Mungu, idara ya wahadhiri wa kike katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya tukio hilo, na kuingizwa katika ratiba ya mwezi wa Ramadhani inayo tekelezwa asubuhi na jioni kila siku katika sardabu ya Alqamiy, wameshiriki wanafunzi na mazuwaru kwenye hafla hiyo.