Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwake: Imepeperuswa bendera ya Imamu Hassan (a.s).

Maoni katika picha
Kamati inayo simamia kongamano la kuzaliwa kwa mkarimu wa Ahlulbit Imamu Hassan Almujtaba (a.s) imezowea kuanza ratiba yake kwa kupandisha bendera ya muadhimishwaji, ya rangi ya kijani iliyo andikwa (Yaa karimu Ahlulbait), inapandishwa katika nguzo iliyopo katika maqaam ya Radu-Shamsi ya Imamu Ali (a.s) katika mji wa Hilla, ambapo hufanywa kongamano kila mwaka, ni ishara ya kuonyesha kudhulumiwa kwake na sehemu ya utamaduni wa kufunguliwa kwa kongamano kubwa kuhusu kuzaliwa kwake, hili ni kongamano la kitamaduni ambalo hufanywa kila mwaka katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), ambalo husimamiwa na watu wa mji wa Hilla kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu ya Husseiniyya na Abbasiyya.

Rais wa kamati inayo simamia kongamano Ustadh Hassan Ali Alhilliy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Madam kuna bendera ya Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Jawadiyya, Radhwawiyya, Abbasiyya katika malalo zao (a.s), hakika tunatamani kuona bendera ya Hassaniyya inapepea juu ya kubba la malalo yake kwenye mji wa Madina, hivyo kila mwaka sisi hupandisha bendera zake mbili katika mji wa Hilla, moja katika kumbukumbu ya kifo chake mwezi wa Safar ambayo ni nyeusi na nyingine ya kukumbuka kuzaliwa kwake ambayo imepandishwa mahala hapa”.

Akaongeza kua: “Tukio hili la kiroho na kiimani limepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wahudhuriaji na washiriki wa kongamano kwa ujumla, huangalia kwa macho yao upandishwaji wa bendera katika sehemu hii ya Radu-Shamsi ya kiongozi wa waumini (a.s) katika mji wa Hilla”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: