Kufuatia kauli ya muadhimishwaji Imamu Hassan (a.s) isemayo: (Haijabaki katika dunia kimbilio zaidi ya Quráni, ifanyezi Imamu itakuongozeni katika uongofu, mwenye haki zaidi na Quráni ni yule atakaye ifanyia kazi hata kama hajaihifadhi, na aliye mbali nayo zaidi ni yule asiyeifanyia kazi hata kama anaisoma), bado usomaji wa Quráni unaofanywa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi unaendelea na kushuhudia ongezeko kubwa la wasomai.
Maahadi ya Quráni tukufu haijatosheka na kuandaa misahafu pamoja na sehemu ya kusomea peke yake, bali imekua ikiwakumbusha wasomaji baadhi ya minasaba (matukio) yaliyo tokea katika mwezi huu, ikiwa ni pamoja na tukio la kuzaliwa kwa mkarimu wa Ahlulbait (a.s) Abu Muhammad Hassan Almujtaba (a.s), wamesambaza misahafu pamoja na vipeperushi vinavyo zungumzia tukio hilo, sambamba na kuonyesha uhusiano baina ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na Quráni tukufu, kwani wao ndio usia wa Mtume (s.a.w.w) kwa umma huu.