Mihadhara mbalimbali ya Dini inatolewa kila siku katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba maalum ya mwezi wa Ramadhani inayo lenga kuwapatia waumini kila kinacho wafaa katika Dini, imani na tabia, Atabatu Abbasiyya tukufu jioni ya kila siku katika mwezi wa Ramadhani inatoa mawaidha baada ya swala ya Magharibaini.

Mawaidha hayo hutolewa na Shekh Swahibu Twaaiy kiongozi wa Maahadi ya Imamu Hassan (a.s) chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, huzungumza mada mbalimbali zinazo husu wailamu kwa ujumla pamoja na kuzungumza mambo yanayo husu funga.

Hali kadhalika huzungumzia mambo mbalimbali yaliyo tokea katika mwezi wa Ramadhani, kama kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) na kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), mawaidha hayo huhudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru wanao fanya ibada zao ndani ya harama tukufu, vilevile hurushwa katika luninga (tv) mbalimbali ili kufikia idadi kubwa zaidi ya waumini na wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbait (a.s) walio enea kila sehemu ya dunia.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba maalum ya mwezi wa Ramadhani, inayo husisha kuimarisha ulinzi na usalama na kutoa huduma kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, inayo endana na utukufu wa mwezi huu, kwa ajili ya kuhakikisha inatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wanaokuja katika Ataba tukufu za Karbala, kwakua malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ni eneo la pili kwa umuhimu linalo kusudiwa na watu wanaokuja kufanya ziara kwa ndugu yake Imamu Hussein (a.s), nayo ni mlango wa utukufu na utowaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: