Dongoo za kihistoria: Mwezi kumi na saba Ramadhani ilipiganwa vita ya Badri na kuonekana utukufu wa kiongozi wa waumini (a.s).

Maoni katika picha
Usiku na mchana wa mwezi kumi na saba Ramadhani unatukio kubwa kwa waislamu wote, tukio la vita ya Badri ambayo ni vita ya kwanza kati ya waislamu na makafiri wa kikuraishi, nayo ni vita mashuhuri zaidi iliyo ongozwa na Mtume (s.a.w.w) dhidi ya makafiri, ina nafasi ya pekee katika historia ya kiislam ukilinganisha na vita zingine, wapiganaji (mujahidina) walio shiriki katika vita hiyo walionyesha Imani na utiifu mkubwa, historia imeandika ushujaa wao.

Baada ya Mtume (s.a.w.w) kufahamu idadi ya wanaeshi wa makuraishi na viongozi wao… aliwaambia wapiganaji wake walio kuwa wachache na wenye siraha duni ukilinganisha na jeshi la makuraishi, Mtume (s.a.w.w) akasema: (watu wa Maka wamekuja na makamanda wao)…, vita ikaanza Ali (a.s) akaenda kupambana nao, wakazuwia visima vya Badri, wakapigana vita kali… ikaja amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu Malaika wakapigana kuwasaidia waislamu, waislamu wakawashinda washirikina, Mwenyezi Mungu akawanusuru waumini, Imani ya waumini ikaongezeka katika nyoyo zao na kuonekana katika macho yao… panga za waislamu zikawafyeka washirikina, upanga wa Dhulfikaar uliuwa nusu ya washirikina walio uwawa katika vita hiyo… makuraishi wakahuzunika sana kwa watu wao walio kufa na wakaweka kisasi dhidi ya Mtume na maswahaba zake…

Waislamu walishinda kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na wakaendelea kupata nguvu na kuheshimika katika nchi zote za uarabuni… ikawa imechomoja nyota mpya ya uongozi katika nchi za uarabuni, watu wa mbali na wakaribu wakaanza kutafakari kuhusu serikali mpya, mkataba wa Madina ulikua ndio katiba kubwa ya utawala huo, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwanusuru. Na yeye ndiye wakutegemewa.

Usiku wa kuamkia siku ya vita, imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kua, aliwaambia maswahaba zake usiku wa Badri: Nani ataenda katika kisima cha Badri atuletee maji? Wakakaa kimya hakuna aliye itika, kiongozi wa waumini (a.s) akachukua kiriba (chombo) na kuelekea kisimani kuchota maji, ulikua usiku wa giza wenye baridi na uprpo mkali, akaenda hadi kisimani, kilikua kirefu na chenye giza nene wala hakua na ndoo ya kuchotea maji, ikamlazimu aingie kisimani akachota maji na kujaza chombo chake kasha akatoka na akaanza kurudi, akapigwa na kimbunga kikali, akakaa chini hadi kilipo tulia, akasimama na kuendelea na safari, kisha kikaja kimbunga kama cha mara ya kwanza, akakaa chini hadi kilipo tulia, akasimama na kuendelea na safari, kikaja tena kwa mara ya tatu, akakaa chini hadi kilipo tulia, akasimama na kuendelea na safari hadi kwa Mtume (s.a.w.w), Mtume akamuuliza: Ewe Abu Hassan kwa nini umechelewa? Akasema (a.s): nimepigwa na kimbunga mara tatu, kila mara ilinilazimu nikae hadi kitulie, Mtume (s.a.w.w) akasema: Je ulitambua vimbunga hivyo ni kina nani ewe Ali? Akasema (a.s): hapana. Mtume (s.a.w.w) akasema: kimbunga cha kwanza alikua ni malaika Jibrilu (a.s) akiwa na malaika elfu moja alikutolea salamu na malaika aliokua nao pia wakakutolea salam. Kimbunga cha pili alikua ni malaika Mikaeli akiwa na malaika elfu moja, pia walikutolea salam. Na cha tatu ni malaika Israfiil akiwa na malaika elfu moja nao walikutolea salamu. Wamekuja kutusaidia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: