Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya kimefungua maonyesho mapya ya vitabu, katika uwana wa katikati ya haram mbili tukufu kwenye eneo la mlango wa Swahibu Zamaan (a.f), kama sehemu ya kufundisha utamaduni wa kiislamu katika sekta mbalimbali, sambamba na maendeleo ya kitamaduni na kielimu.
Maonyesho yanahusisha idadi kubwa ya vitabu vilivyo andikwa na kitengo hicho pamoja na vitengo vilivyo chini yake, pia kuna makumi ya vitabu, majarida na vipeperushi kuhusu adabu, mashairi, elimu ya nafsi (saokolojia), jamii, lugha, historia na mengineyo, pamoja na vitabu vya dua, ziara na Quráni, vitabu vingine vimechukuliwa kutoka taasisi ya usambazaji wa vitabu nchini Iran, Lebanon na nchi zingine, vimechapishwa kuwa ukubwa na viwango tofauti.