Kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s): Hafla ya usomaji wa mashairi jirani na malalo mawili ya ndugu zake (a.s).

Maoni katika picha
Katika mazingira yaliyojaa shangwe na furaha jirani na malalo ya ndugu zake, Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi (a.s), wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wana adhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), chini ya uratibu wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu kwa kufanya hafla ya usomaji wa mashairi ambayo wameshiriki washairi kadhaa na waimbaji, na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya waumini na mazuwaru wa Ataba mbili tukufu.

Hafla ilifunguliwa kwa Quráni tukufu na surat Fathwa kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha yakasomwa mashairi pamoja na kaswida mbalimbali, zinazo onyesha mapenzi na kushikamana na Mtume pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s), walipaza sauti zao na kuonyesha mapenzi ya dhati kwa Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake (a.s) hususan Imamu Hassan Almujtaba (a.s) aliye angazia dunia kwa kuzaliwa kwake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: