Katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s): Usiku wa Ijumaa ya tatu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani watu wamiminika kwa wingi.

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya baada ya Adhuhuri ya Alkhamisi mwezi kumi na saba Ramadhani, zimeshuhudia ongezeko kubwa la watu wanaokuja kutembelea malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), huku ulinzi ukiwa umeimarishwa na watumishi wa Ataba mbili wakiwa wameboresha huduma na kuwapatia mahitaji yote muhimu.

Watu walianza kumiminika kwa wingi baada ya Alasiri na wakaendelea hadi wakati wa Magharibaini na baada yake hadi Alfajiri ya siku ya Ijumaa.

Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanafanya kazi kwa imani kubwa chini ya ratiba iliyo pangwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya mwezi huu, wanafanya kila wawezalo kwa ajili ya kuhakikisha mazuwaru wanafanya ziara na ibada kwa amani na utulivu
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: