Kwa picha: Katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ibada za kuhuisha usiku wa kwanza wa Lailatul-Qadri na kukumbuka kujeruhiwa kwa mzazi wake (a.s).

Maoni katika picha
Mazingira ya kiroho na kiimani ya Lailatul-Qadri ni kusudio la kila muumini anayetaka kupata radhi za Mwenyezi Mungu na usaidizi wake, jirani na malalo takasifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) waumini wamefanya ibada za usiku wa kwanza wa Lailatul-Qadri, pamoja na kukumbuka tukio la kujeruhiwa kwa kiongozi wa waumini (a.s).

Haram imefurika waumini katika usiku huu mtukufu, wamekesha wakiswali tahajudi na kuomba dua, ikiwemo dua ya kuinua misahafu pamoja na kusoma dhikri mbalimbali ambazo ni maalum kwa usiku huu, wakiwa na matumaini ya kukubaliwa ibada zao na Mwenyezi Mungu mtukufu pamoja na kusamehewa dhambi zao na kuachwa huru na moto.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu katika ratiba yake ya mwezi wa Ramadhani iliweka vipengele maalumu vya siku hizi –kukumbuka kifo cha kiongozi wa waumini (a.s) na ibada za siku za Lailatul-Qadri- na kuingizwa katika ratiba ya mihadhara ya mwezi wa Ramadhani inayo tolewa kila siku kuzungumzia mambo yanayo husu siku hizi, kuanzia siku aliyo jeruhiwa Imamu Ali kiongozi wa waumini hadi siku ya kifo chake (a.s), katika siku hizo pia kila baada ya muhadhara husomwa maatam, kila kinacho hitajika na zaairu kwa ajili ya kufanya ibada kimeandaliwa.

Usiku wa mwezi kumi na tisa ndio usiku wa Lailatul-Qadri ya kwanza, Lailatul-Qadri ni usiku usio fananishwa na usiku wowote kwa utukufu, kufanya ibada katika usiku huo ni bora kushinda kufanya ibada miezi elfu moja, katika usiku huo hukadiriwa mambo ya mwaka mzima, hushuka malaika kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na kupita mbele ya Imamu wa zama (a.s) na kumuonyesha makadirio ya kila mtu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: