Mtandao wa kimataifa Alkafeel unatoa wito kwa wapenzi na wafuasi wote wa Ahlulbait (a.s) kote duniani waishio mbali na (Ataba tukufu za Iraq) na hawajaweza kuja, wasajili majina yao kwa ajili ya kufanyiwa ibada za masiku ya Lailatul-Qadri na ziara ya Imamu Ali (a.s) kwa niaba yao, pamoja na ibada zingine za mwezi mtukufu wa Ramadhani zilizo kwisha tangazwa, kama ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kusoma dua ya Iftitaah na zinginezo.
Mtandao umeandaa watu maalum kwa ajili ya kufanya ibada za ziara na dua kwa niaba ya kila atakae sajili jina lake kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba kupitia linki ifuatayo: (http://alkafeel.net/zyara).