Je Atabatu Abbasiyya tukufu imepata ufumbuzi kuhusu kupungua kwa maji ya mto wa Furat?

Maoni katika picha
Mradi wa kutumia maji mbadala unafanyika kupambana na tatizo la upungufu wa maji ambalo limeanza kuenea duniani kwa ujumla pamoja na Iraq kutokana na uharibufu wa vyanzo vya maji ya mto Dujla na Furat, hivyo ni muhimu kuanza kutumia maji mbadala yatokanayo na visima, Atabatu Abbasiyya tukufu imeamua kutekeleza mradi wa kuchimba visima kwa kushirikiana na idara za serikali za mkoa pamoja na ofisi za kilimo na visima.

Nao ni miongoni mwa miradi muhimu katika mkoa wa Karbala pamoja na Iraq kwa ujumla, utasaidia sekta ya kilimo cha chakula kwa watu wa Karbala na mikoa mingine ya Iraq ya kusini, upatikanaji wa maji ya visima utasaidia pindi maji ya mto yatakapo kauka kwani visima ni hazina kubwa ya maji na inatakiwa itumiwe vizuri.

Haikuishia kuchimba visima peke yake bali kuna miradi mingine, kama kujenga kituo kikubwa cha kusafisha maji, na kituo cha mitambo ya kuendesha mradi huo pamoja na kulima baadhi ya mazao adim na tende.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: