Maneno bora ya kuanza nayo kumuelezea kiongozi wa waumini (a.s) katika siku ya kukumbuka kifo chake ni maneno aliyo sema Mtume (s.a.w.w) akimsifu kwa kusema: (Atakayetaka kuangalia utukufu wa Adam, na hekima ya Shithi, na haiba ya Idrisa, na shukrani ya Nuhu pamoja na ibada zake, na uaminifu wa Ibrahim, na hasira za Mussa kwa kila adui wa Mwenyezi Mungu, na mapenzi ya Issa kwa waumini wake na namna alivyo ishi nao, amwangalie Ali bun Abu Twalib). (Biharul-Anwaar cha Majlisiy: jz 17: uk 419, ml 5 hdth 49).
Katika hadithi nyingine Mtume (s.a.w.w) akasema: (Anayetaka kuangalia uzuri wa Yusufu, na unyenyekevu wa Ibrahim, na tabasamu ya Suleiman, na hekima ya Daudi, amwangalie Ali bun Abu Twalib). (Biharul-Anwaar cha Majlisiy: jz 39, uk 35, ml 73 hdth 2).
Akasema (s.a.w.w) kumwambia Ali (a.s): (…Lau sio kuhofia watu katika umma wangu wasije kusema kuhusu wewe kama walivyo sema manaswara kwa Issa mwana wa Maryam, ningesema neno kuhusu wewe usingepita sehemu yeyote ispokua watu wangechukua udongo wa nyayo zako wakiutumia kupata Baraka…). (Alkafi cha Shekh Kuleini: jz 8, uk 57).
Amesema (s.a.w.w): (Ewe Ali hakuna amjuae Mwenyezi Mungu ukweli wa kumjua ispokua mimi na wewe na hakuna akujuae ispokua Mwenyezi Mungu na mimi). (Almanaqib cha ibun Shahari Ashuub: jz 3, uk 60).
Haya ni baadhi ya yaliyosemwa kuhusu wasifu wa kiongozi wa waumini (a.s) naye ni waliy mkuu wa Mwenyezi Mungu na kiongozi wa binadamu, maneno haya kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ni dalili ya wazi kua yaliyo semwa na kuandikwa na yatakayo semwa na kuandikwa kuhusu Ali ni madogo sana sawa na mbu mbele ya ukuu wa Mwenyezi Mungu.
Kila mwaka waumini hufanya ibada za usiku wa mwezi ishirini na moja Ramadhani unaosadifu siku ya kifo chake mbele ya kaburi lake tukufu, Atabatu Alawiyya tukufu hufurika watu wanao rukuu, kusujudu na kusoma kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu.