Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya majlisi za kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).

Maoni katika picha
Kutokana na kumbukumbu ya kifo cha kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) na kwa mujibu wa ratiba ya msiba huu, Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya siku tatu (19, 20, 21) Ramadhani, imefanya majlis za maombolezo kwa wafanya kaziwa wake ndani ya ukumbi wa utawala, nao ni utamaduni ulio zoweleka katika kuomboleza misiba ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Majlisi hizo zilikua zikihutubiwa na mmoja wa Mashekh kutoka kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kila siku majlisi ilifunguliwa kwa Quráni tukufu, kisha inafuata mada maalum kuhusu mbora wa mawasii Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), ambapo mzungumzaji alikua anaeleza maisha ya Imamu (a.s) na utukufu wake pamoja na madhila aliyofanyiwa (a.s), pia alieleza ibada zake na ushujaa wake sambamba na namna alivyo simama imara pamoja na Mtume (s.a.w.w) katika matukio mengi, kwa nini asiwe hivyo wakati yeye ni mtu wa karibu zaidi na Mtume na mtoto wa ammi yake na mume wa binti yake, pia mzungumzai alieleza maisha ya Imamu Ali yaliyojaa ibada na tabia njema.

Mwisho majlisi zilikua zinafungwa kwa kaswida zinazo elezea kifo cha Abu Hassanain (a.s) kazika mazingira yaliyojaa huzuni kubwa, huku watu wakitokwa machozi na kulia kutokana na msiba huo uumizao nyoyo za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: