Kwa ushiriki wa watu (128) kutoka nchi (68) kwenye mashindano ya Quráni: Mmoja wa wanafunzi wa Maahadi ya Quráni amepata nafasi ya nne katika mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Quráni na usomaji bora.

Maoni katika picha
Abdullahi Zuhair Alhusseiniy mmoja wa wanafunzi wa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Hindiyya na mshiriki wa mradi wa kuandaa wasomi wa kitaifa unao endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, amekua mshindi wa nne katika mashindano ya usomaji wa Quráni, kwenye mashindano ya saba ya kimataifa ya kuhifadhi Quráni na usomaji bora yaliyo fanyika nchini Uturuki katika jiji la Stambuul kati ya washiriki (128) kutoka nchi (68).

Fahamu kua mashindano hayo yanasimamiwa na mamlaka ya Dini ya Uturuki na hufanywa kila mwaka, nchi mbalimbali hushiriki katika mashindano hayo, hupitia mizunguko ya kutowana hadi kufikia katika mzunguko wa mwisho ulio toa matokeo hayo.

Kumbuka kua wasomaji wa Quráni kutoka Maahadi ya Quráni ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamesha pata ushindi katika mashindano mengi ya kitaifa na kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: