Kwa maukibu ya kuomboleza ya pamoja: watumishi wa Ataba mbili tukufu wampa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi katika kumbukumbu ya kifo cha baba yake kiongozi wa waumini (a.s).

Maoni katika picha
Kwa majonzi na huzuni kubwa baada ya Adhuhuri ya Jumanne (21 Ramadhani 1440h) sawa na (27 Mei 2019m) watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wamefanya maukibu ya pamoja, kuomboleza kifo cha mbora wa mawasii na kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), kwa ajili ya kutoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na Imamu wa zama (a.f) kutokana na msiba mkubwa uliotokea katika umma wa kiislam.

Maukibu ilianzia katika uwanja wa haram ya Abbasi, baada ya kumpa pole Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakipiga vifua na kulia pamoja na kuimba kaswida za maombolezo, zilizo onyesha ukubwa wa msiba uliotokea katika umma wa Muhammad, walipofika kwenye haram ya Imamu Hussein (a.s), ndugu zao watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu wakawapokea, kisha wakafanya majlisi ya pamoja ambayo idadi kubwa ya mazuwaru walishiriki pia.

Fahamu kua maukibu ya kuomboleza ya pamoja kati ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, ni sehemu ya ratiba maalum ya Ataba mbili katika kila tukio la huzuni kwa watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: