Tawi la Maahadi ya Quráni katika mkoa wa Baabil linasimamia zaidi ya vituo (23) vya usomaji wa Quráni.

Maoni katika picha
Katika kufaidika na siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kusoma Quráni tukufu na kufanya tafakuri na mazingatio kwa namna ambayo mtu anaongeza uongofu na nuru, na kufanyia kazi kauli ya Imamu Baaqir (a.s) isemayo: (Kila kitu kina msimu na msimu wa Quráni ni mwezi wa Ramadhani), ndipo Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Bagdad (Shaáb) chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu likasimamia zaidi ya vituo (23) vya usomaji wa Quráni ndani ya mwezi huu mtukufu katika mkoa wa Baabil.

Vikao vya usomaji wa Quráni ni moja ya harakati zinazo fanywa na Maahadi katika utaratibu wake makhsusi wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, visomo hivyo hufanywa misikitini na katika husseiniyya zilizopo kila mahala, na huongozwa na wasomaji mahiri wa Quráni kwa ushiriki wa kundi kubwa la waumini, kwa kufuata maelekezo ya Atabatu Abbasiyya yanayo lenga kueneza utamaduni wa Quráni katika jamii.

Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu inasimamia vikao vingi vya usomaji wa Quráni katika mkoa wa Karbala na mikoa mingine, kwa ajili ya kutengeneza kizazi chenye kufuata maadili ya Quráni tukufu na kizazi kitakatifu, Maahadi inatekeleza ratiba maalum katika mwezi wa ramadhani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: