Kutokana na kumbukumbu ya kifo cha baba wa mayatima Imamu Ali (a.s), na muengelezo wa ratiba ya kushirikiana na taasisi zinazo lea mayatima, imekaribisha zaidi ya mayatima (200) pamoja na walezi wao, kwa kushirikiana na taasisi ya Nurul-Hussein (a.s) Alkhairiyya hapa Karbala.
Wamewekewa ratiba maalum inayo husisha kuzuru haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuwatembeza katika korido za Ataba tukufu, baada ya hapo wakakaribishwa katika mgahawa na kupewa futari ya pamoja.
Asilimia kubwa ya mayatima hao ni watoto wa wapiganaji wa Hashdi Shaábi na familia masikini, wamefurahi na kushukuru sana jambo hili lililo fanywa na Ataba tukufu.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba maalum ya mwezi wa Ramadhani yenye vipengele vingi kikiwemo kipengele hiki.