Kwa picha: Uhuishaji wa Lailatul-Qadri katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Jirani na haram tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mazingira ya kiroho na kiimani waumini wamefanya ibada za usiku wa tatu wa Lailatul-Qadri.

Uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umejaa watu wanaofanya ibada katika usiku huu mtukufu, wameswali tahajudi na kusoma dua ya kuinua misahafu pamoja na kusoma Quráni na nyeradi mbalimbali za usiku huu, wakiwa na matumaini makubwa ya kukubaliwa toba zao katika eneo hili takatifu na kuachwa huru na moto.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kufanya ibada katika masiku haya ya Lailatul-Qadri, imeweka mazingira mazuri ya kiroho pamoja na kuweka vitu vyote muhimu vinavyo hitajika na mazuwaru, sambamba na kubeba mazuwaru kuwatoa sehemu moja hadi nyingine na kuongeza miamvuli nje ya haram pamoja na mabusati na maji, sambamba na kutumia sehemu zilizo ongezwa.

Mji mtukufu wa Karbala umeshuhudia ongezeko kubwa la mazuwaru kutoka ndani na nje ya mji huu mtukufu waliokuja kufanya ibada ndani ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na katika Husseiniyya mbalimbali, wameswali, kusoma Quráni na dua, pia kuna harakati tofauti zilizo fanyika katika kuwahudumia mazuwaru watukufu ndani ya mji mtukufu wa Karbala na kwenye Ataba takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: