Maahadi ya Qur’ani tukufu imetangaza kuanza kwa usajili wa kozi za Qur’ani za majira ya joto (kiangazi).

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza tarehe ya kuanza usajili wa kozi za Qur’ani za kipindi cha majira ya joto (kiangazi) masomo yatakayo fundishwa ni Qur’ani, fiqhi, Akhlaq na Aqida.

Umri wa washiriki ni kati ya miaka (6) hadi (16), wanafunzi wa darasa la kwanza hadi darasa la nne wa shule za msingi, usajili inafanyika makao makuu ya Maahadi katika mji mtukufu wa Karbala karibu na haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mkabala na mlango wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s), usajili unafanyika kwa kujaza fomu na kuambatanisha na kitambulisho cha uraia, usajili utaanza (1 Juni) hadi (10 Juni 2019m).

Kumbuka kua kozi hizi zinalenga kufundisha Qur’ani ikiwa ni sehemu ya kufanyia kazi hadithi ya Mtume isemayo: (Wafundisheni watoto wenu mambo matatu: Kumpenda mtume wenu, kuwapenda Ahlulbait wake na kusoma Qur’ani), hutolewa kila mwaka kipindi cha likizo, maelfu ya wanafunzi wamesha hitimu kozi hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: