Kwa picha: Muonekano wa mwisho wa mradi wa kituo cha cha kisasa cha maegesho ya magari cha Alkafeel, moja ya miradi mikubwa hapa Iraq.

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesema: “Mradi wa kituo cha kisasa cha kuegesha magari umefika hatua ya mwisho, siku chache zijazo utakua tayali kwa ufunguzi, bado tunaendelea kumalizia baadhi za sehemu, kwa kufuata utaratibu ulio wekwa pia tutamaliza ndani ya muda ulio pangwa, kwa kiwango ambacho kimejengwa kwa mara ya kwanza hapa Iraq”.

Akaongeza kua: “Hakika huu ni miongoni mwa miradi muhimu na mkubwa kutekelezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, unaendana na malengo yaliyo pangwa, ni moja ya sehemu muhimu katika mkoa wa Karbala”.

Kumbuka kua kituo cha kisasa cha kuegesha magari ni kituo cha mara ya kwanza cha aina hii kujengwa hapa Iraq, kimejengwa katika kiwanja chenye ukubwa wa (2m72.125) ukubwa wa jengo ni (mita za mraba 142,000) limegawanywa sehemu tano:

  • 1- Jengo la utawala: nalo ndio makao makuu ya mradi, kuna ofisi zinazo andika taarifa za vyombo vya usafiri vyote vinavyo ingia katika eneo hilo.
  • 2- Kituo cha mafuta: kinafanya kazi ya kuweka mafuta kwenye vyombo vya usafiri, kina hazina ya lita (1,000,000) na kina mitambo ya kisasa.
  • 3- Jengo la kutengeneza vyombo vidogo vya usafiri (gereji ya magari madogo).
  • 4- Jengo la kutengeneza vyombo vikubwa vya usafiri (gereji ya magari makubwa).
  • 5- Jengo la ghorofa mbili la kuegesha magari madogo na makubwa, linye uwezo wa kuegesha gari (500) limejengwa kisasa zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: