Kuhuisha siku tukufu: Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wa kike imeweka ratiba kwa wanawake ya kufanya ibada za mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutekeleza ratiba ya mwezi wa Ramadhani, kadri mwezi unavyo karibia kuisha ndio inavyo zidi kupata mwitikio, imepata mahudhurio makubwa sana katika siku za Lailatul-Qadri na baada yake, ratiba ya ibada inaendana na utukufu wa siku hizi, wanawake wengi kutoka ndani na nje ya Karbala wameshiriki katika ratiba hiyo, pamoja na mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Ustadhat Taghrida Abdulkhaaliq Tamimi makamo kiongozi wa idara ya wahadhiri wa kike ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu ratiba hiyo: “Ratiba ya mwezi wa Ramadhani iliyo andaliwa na idara yetu kwa ajili ya kufanya ibada za mwezi mtukufu wa Ramadhani inavipengele vingi, ikiwa ni pamoja na kipengele cha ibada za siku za Lailatul-Qadri zilizo husisha usomaji wa Qur’ani, dua ya Iftitaah na ibada zingine ambazo ziliendelea hadi Alfajiri, ziliongozwa na Shekhe kutoka kitengo cha Dini, na kugawa daku kwa washiriki wa ibada hizo, ni matumaini yetu wamenufaika kwa kiwango kikubwa”.

Akasisitiza kua: “Mwitikio ulikua mkubwa, Sardabu ya Alqamiy ndani ya jengo la Atabatu Abbasiyya ilijaa watu, jambo ambalo linashajihisha kupanua ratiba hii siku za mbele”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: