Nyoyo zilizo jaa Imani ya Rahmani, zinaelekea katika mlango wa Mwenyezi Mungu ambao hutolea (rehma zake), kufanya ibada za usiku wa Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani.
Pamoja na joto kali la jua, waumini wametembea kuelekea katika eneo takatifu la haram ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kufanya ibada na kuzitakasa nafsi katika siku ambayo haitarudi tena hadi baada ya mwaka.
Atabatu Abbasiyya tukufu imeimarisha ulinzi na utowaji wa huduma ili kuwawezesha kufanya ibada kwa Amani na utulivu, inatarajiwa kuendelea kuongezeka idadi yao kadri muda wa swala ya Maghribaini unavanyo sogea.
Kamera ya Alkafeel imeshuhudia jinsi watu wanavyo miminika katika mji mtukufu wa Karbala na inakuletea baadhi ya picha.