Katika mazingira bora ya kiroho yanayo endana na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), ndani ya ukumbi mtakatifu na wenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), waumini kutoka ndani na nje ya Iraq wamekesha wanafanya katika usiku wa Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Korido na uwanja wa haram ya Abbasiyya umejaa watu wanaofanya ibada mbalimbali, watu hao wameamua kuutumia usiku huu kwa kufanya ibada ndani ya eneo hilo tukufu, hakika Mwenyezi Mungu mtukufu katika kila siku ya mwezi wa Ramadhani wakati wa futari huwaacha huru na moto watu elfu elfu (1,000,000), itakua vipi kwa wale wanaokesha katika usiku huu mtukufu mahala patakatifu kwa ajili ya kuonyesha mapenzi kwa Mwenyezi Mungu na kumuabudu, tena wakiwa jirani na bwana wa mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Watumishi wa Ataba mbili tukufu wamefanya kila wawezalo kuweka mazingira mazuri yatakayo wawezesha mazuwaru kufanya ibada kwa amani na utulivu, ibada zao zilianza kwa kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), vikosi vya ulinzi na usalama vimeimarisha usalama maeneo yote hasa katika barabara kubwa na ndogo zinazo elekea kwenye Ataba tukufu.