Maandalizi ya kufanya kongamano la awamu ya nne la fatwa tukufu ya kujilinda yanaendelea.

Maoni katika picha
Maandalizi ya kufanya awamu ya nne ya kongamano la kuadhimisha fatwa ya kujilinda yanaendelea vizuri, litakalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni chini ya kauli mbiu isemayo: (Nyie ni fahari yetu na utukufu wetu na mnapongezwa na kila umma), litakalo anza (25 Shawwal 1440h) sawa na (28 Juni 2018m), ikiwa ni kuadhimisha mwaka wa tano tangu kutolewa kwa fatwa tukufu ya jihadi kifaya ya kulinda taifa la Iraq na maeneo matakatifu, kwa ajili ya kuenzi ushujaa ulio onyeshwa na raia wa Iraq walio pambana hadi wakawashinda magaidi wa Daesh.

Kamati ya maandalizi imeendelea kuchambua vitu vilivyo wafikia vitakavyo shiriki katika mashindano mbalimbali yatakayo fanyika katika kongamano hilo, mashindano hayo ni:

Kwanza: Shindano la filamu bora.

Pili: Shindano la picha za mnato.

Tatu: Shindano la makala bora kuhusu fatwa tukufu ya kujilinda na ujasiri wa Hashdi Sha’abi.

Nne: Shindano la kisa kifupi.

Tano: Shindano la kazi za mikono (uchoraji na uchongaji).

Sita: Shindano la kisa kifupi cha watoto.

Hali kadhalika kutakua na kauli mbiu isemayo (Marjaiyya Diniyya ni ngao madhubuti ya umma wa kiislamu) chini ya anuani isemayo: (Fatwa tukufu ya kujilinda baina ya kale na sasa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: