Mafundi wa kiwanda cha Saqaa wameanza kazi katika hatua ya kwanza ya kuweka dhahabu sehemu ya juu ya dirisha la Maimamu wawili Aljawadaini (a.s).

Maoni katika picha
Mafundi na wahandisi wanaofanya kazi katika kiwanda cha Saqaa cha kutengeneza madirisha na milango ya makaburi na mazaru chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wameanza hatua ya kwanza ya kuweka dhahabu sehemu ya juu ya dirisha tukufu la kaburi la maimamu wawili Aljawadaini (a.s).

Sehemu ya kwanza ya kazi hiyo ni kubaini kila kipande cha sehemu ya juu, pamoja na kukipa namba, kisha namba hizo zikakusanywa katika masanduku maalum, kila namba ikiwa na vipimo kamili vya sehemu yake, kwa ajili ya kuzipeleka kiwandani na kuingia katika hatua ya pili ya utendaji, baada ya kuondoa sehemu zilizo chafuka na zilizo haribika inafuata kazi ya kuweka vipande vya dhahabu kwa ustadi wa hali ya juu na kisasa zaidi.

Kumbuka kua mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaofanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza madirisha ya kwenye makaburi na mazaru, wana uzowefu mkubwa wa kufanya kazi hiyo, wameonyesha umahiri na mafanikio katika miradi mingi ikiwa ni pamoja na mradi wa kutengeneza dirisha la kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), nalo ndio dirisha la kwanza kusanifiwa na kutengenezwa na mikono ya wairaq, kisha wakatengeneza dirisha la Qassim (a.s) na milango ya malalo ya Sayyid Muhammad –Sab’u Dujail- na madirisha ya Swafi Swafa bila kusahau madirisha ya malalo ya Shekh Mufid na Shekh Tusi (q.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: