Ni upi ukweli wa gharaba za hospitali ya rufaa Alkafeel? Na mapato yake yanakwenda wapi?

Maoni katika picha
Idara ya hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza sababu za ongezeko la gharama za upasuaji, imesema kua mapato yake yanatumika kulipa watumishi na kusaidia wagonjwa mafakiri, na baadhi ya mapato yake yanakwenda serikalini kusaidia huduma za maji na umeme pamoja na vitu vingine, sambamba na kulipa pamenti na bima za madaktari wa kigeni.

Imebainisha kua: “Kuongezeka kwa gharama za upasuaji kunatokana na kuongezeka kwa bei za vifaa vya kisasa vinavyo tumika kimataifa katika upasuaji, huduma hii inatakiwa kuwa endelevu hivyo inahitaji hela nyingi, kwani upasuaji wowote unaofanywa hapa hospitalini hufanywa na madaktari bingwa ambao wanatakiwa kulipwa, nao wanatoka ndani na nje ya Iraq”.

Ikafafanua kua: “Sehemu ya pili ya pesa inayo tolewa na mgonjwa inatumika kulipa mishahara ya madaktari na wauguzi pamoja na kulipia umeme na maji na vitu vingine vinavyo tumika katika jengo la hospitali, pia zinatumika kulipia tiketi, pamenti na bima za madaktari wa kigeni, sehemu ya hela inayo bakia inasaidia katika mradi wa (matibabu bila malipo) unao lenga kusaidia familia za mafakiri na Hashdi Sha’abi pamoja na mradi wa (punguzo) ambalo hupewa wagonjwa mafakiri ambao hupunguziwa nusu ya bei au hutibiwa bure kabisa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: