Vipengele muhimu alivyo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa.

Maoni katika picha
Katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) leo (25 Ramadhani 1440h) sawa na (31 Mei 2019m) chini ya uimamu wa Sayyid Ahmadi Swafi Marjaa Dini mkuu ameogea vipengele vingi vya kimaadili na kimalezi vinavyo endana na mazingira halisi tunayo ishi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

 • - Tunashuhudia ukatili na kutenzana nguvu katika jamii zetu zinapo taka kutatua tatizo.
 • - Utumiaji wa nguvu huongeza tatizo.
 • - Wakati mwingine unaweza kuamiliana na mtu dhaifu kiafya au kiuchumi isiwe sababu ya kumfanyia ukatili.
 • - Kila tatizo linautatuzi wake jambo la msingi ni kubaini tatizo.
 • - Malezi bora yanatakiwa kuanzia utotoni sote tunajua (kusoma katika utoto ni sawa na kuandika kwenye jiwe).
 • - Zana za malezi zinazo tumika hivi sasa zinachochea ukatili hadi ndani ya familia.
 • - Ushujaa ni maumbile ya kiroho hauna uhusiano na ukatili.
 • - Mtu shujaa ni yule anaye tetea haki yake kwa kutumia hekima na busara.
 • - Kutumia nguvu sio ubinaadamu.
 • - Usimzoweshe mtoto kutumia nguvu dhidi ya wenzake.
 • - Sisi ni umma wenye misingi mizuri ya kimaadili, kwa nini tumeiacha?!
 • - Shule, familia na jamii tusiwalee vijana wetu katika mazingira ya ukatili.
 • - Mitandao ya mawasiliano ya kijamii na luninga (tv) vinachangia kutoa mafundisho ya ukatili.
 • - Kijana anatakiwa kujiamini na kufanya kazi wala sio kukata tamaa.
 • - Kijana yupo katika ulimwengu wa wazi asipo ongozwa anaweza kudumbukia katika matatizo ya kimaadili na kimalezi.
 • - Baadhi ya vijana wanapupia katika kutafuta hela hata kama watazikwaza familia zao na marafiki wao.
 • - Kuna mambo ya ajabu yamezuka katika jamii yetu ambayo hayakuwepo zamani.
 • - Ukatili hauna uhusiano na ushujaa.
 • - Ushujaa ni kitu kingine na ukatili kitu kingine.
 • - Mwanaadamu huwa na amani anapokua na mtu shujaa na hukosa amani anapokua na mtu katili.
 • - Ni vizuri kumlea mtoto katika ushujaa ili awe na faida katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: