Idara ya ustawi wa jamii yaandaa futari ya wanafunzi wa bweni katika chuo kikuu cha Diyala.

Maoni katika picha
Baada ya kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani shughuli mbalimbali za kujitolea zikaanza kufanywa na idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa namna ambayo inaendana na utukufu wa mwezi huu, miongoni mwa shughuli hizo ni hii iliyo fanywa na tawi la mkoa wa Diyala ya kupika futari kila siku kwa ajili ya wanafunzi wa bweni katika chuo kikuu cha Diyala.

Kiongozi wa idara ya ustawi wa jamii katika tawi la mkoa wa Diyala bwana Hassan Mussawi amesema kua: “Hakika mwezi wa Ramadhani una baraka nyingi hazihesabiki, yatupasa kuzichangamkia kadri tuwezavyo katika kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu mtukufu, kwa baraka za mwezi huu na kwa mwaka wa pili mfululizo tumekua tukiwapikia futari wanafunzi wa bweni katika chuo kikuu cha Diyala”.

Akaongeza kua: “Kila siku tunapika sahani (150-200) za futari, asilimia kubwa ya wanafunzi hao wanatoka mikoa ya jirani na ya mbali, halafu wapo katika kipindi cha mitihani, tumeamua kuwaandalia futari kwa ajili ya kuwapunguzia uzito ndani ya mwezi huu wa fadhila”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: