Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa misaada kwa mayatima na familia za masikini.

Maoni katika picha
Miongoni mwa shughuli zake za kibinaadamu kuhusu kusaidia mayatima, Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kuwasaidia kwa kupitia taasisi ya Alfadhil Liriáyatul Aitami, ambayo hutoa mahitaji ya mayatima kama vile chakula, vinywaji na nguo kwa kutumia utaratibu wa kuwapeleka sokoni na wao kuchagua nguo wanazo taka, utaratibu ambao unalinda heshima yao.

Rais wa taasisi Shekh Hussein Turabi ameuambia mtangao wa Alkafeel kua: “Taasisi ya Fadhil Liriáyatul Aitami ni moja ya taasisi zinazo saidia mayatima na familia za mashahidi walio itikia wito wa taifa na Marjaiyya, wakajitolea damu zao takatifu kwa ajili ya kulinda taifa, ikiwa kama sehemu ya kutoa huduma, Atabatu Abbasiyya tukufu imeamua kusaidia kundi hili la watu kwa aili ya kuwapunguzia ugumu wa maisha na kuwasaidia katika kupambana na changamoto za maisha, na kuwaenzi wale walio jitolea damu zao kwa alijili ya taifa hili na Dini”.

Akabainisha kua: “Yametumika magari katika ugawaji chini ya muongozo wa taasisi, majina ya wahusika yalisambazwa katika maduka ya shirika la Nurul-Kafeel huku wahusika wakipewa vitambulisho maalumu vinavyo wawezesha kwenda katika maduka hayo na kuchukua kitu chochote wanacho taka kulingana na pesa zilizopo katika vitambulisho hivyo, pesa walizo kadiriwa ni dinari elfu (30), tumefungua kituo cha kibiashara ambacho wanaweza pia kwenda kuchukua chochote wanacha taka kwa kufuata utaratibu uleule”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: