Zaidi ya upasuaji elfu (38) uliofanywa na hospitali ya Rufaa Alkafeel ndani ya miaka mitatu, umefanikiwa kwa asilimia (%99.36).

Maoni katika picha
Mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Jaasim Ibrahimi amesema kua tangu kufunguliwa kwa hospitali hadi mwezi wa nne mwaka huu (2019m) jumla ya upasuaji wa aina mbalimbali (38.254) umefanywa.

Akaongeza kua: “Kiwango cha mafanikio yaliyo patikana katika upasuaji huo ni asilimia (%99.36) hicho ni kiwango cha juu ambacho hakifikiwi hata hospitali kubwa za kimataifa, hakika tunahaki ya kujivunia mafanikio haya, yanatokana na juhudi za madaktari, wauguzi na idara pamoja na watumishi wote wa kiiraq na wa kigeni, pamoja na uwepo wa vifaa tiba vya kisasa vinavyo endana na maendeleo ya ulimwengu wa kimatibabu wa sasa”.

Akabainisha kua: “Upasuaji ulikua unafanywa na madaktari bingwa wa Iraq na wa kigeni, ikiwa ni pamoja na upasuaji wa moyo, saratani, viungo na nk..”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: