Mawakibu za kutoa huduma za Husseiniyya zinashindana kuwahudumia mazuwaru wa malalo mawili tukufu katika siku za mwezi wa fadhila.

Maoni katika picha
Kama kawaida yao, watoa huduma wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika mji mtukufu wa Karbala, wanashindana kuwahudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kipindi chote cha mwaka, wanatoa huduma wakati wote, kwao kutoa huduma ndio msingi wa maisha yao, hiyo ndio hali ya mawakibu za kutoa huduma za Karbala,

Bwana Riyadhi Ni’mah Salmaan rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ameongea na mtandao wa Alkafeel kua: “Katika siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani mawakibu hugawa futari na chakula kwa mazuwaru, katika njia zinazo tumiwa zaidi na mazuwaru, muda wa kufuturu hutandika vyakula vya aina mbalimbali, hushindana kuwahudumia mazuwaru waliofunga kama wanavyo shindana kuwahudumia mazuwaru katika siku za ziara za milionea ndani ya mwezi wa Muharam na ziara ya Arubaini”.

Akabainisha kua: “Mawakibu Husseiniyya za Karbala pamoja na zile zinazo toka nje ya Karbala zinagawa futari kwa mazuwaru mwezi mzima wa Ramadhani pamoja na aina mbalimbali za matunda sambamba na ugawaji wa chai, kumhudumia zaairu wa Imamu Hussein kwao hakuna muda wala siku, wanatoa huduma kuanzia miezi ya huzuni, Muharam na Safari, na wanaendelea kutoa huduma katika matukio yote ndani ya mwaka mzima”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: