Jopo la wasomi wa sekula na watafiti kutoka Najafu.. miradi ya Atabatu Abbasiyya ni mizuri na inafaa kupongezwa.

Maoni katika picha
Kwa wiki ya pili mfululizo Atabatu Abbasiyya imekaribisha ugeni uliohusisha wanahabari, wasomi wa kisekula, watafiti na viongozi wa taasisi za kiraia kutoka Najafu Ashrafu, waliokuja kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mwenyeji wa ugeni huo Ustadh Farasi Karbasi na rais wa kikosi cha utamaduni ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Ziara hii ni sehemu ya ziara nyingi zinazo fanywa na watu mbalimbali katika Atabatu Abbasiyya nalo sio jambo geni, hivyo tumepokea ugeni kutoka Najafu ulio husisha wasomi wa fani tofauti, wamo wanahabari, wasomi wa kisekula pamoja na wajumbe walio wakilisha kikosi cha utamaduni cha Najafu, wametembelea mradi wa Darul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji pamoja na hospitali ya rufaa Alkafeel”.

Akaongeza kua: “Wageni wametembelea miradi hiyo miwili na kusikiliza maelezo kutoka kwa watendaji wa miradi hiyo kuhusu vifaa walivyo navyo na utendaji wao kwa ujumla”.

Akabainisha kua: “Baada ya kumaliza matembezi yaliyo jaa maswali na ufafanuzi mbalimbali walifanya mazungumzo yaliyo ongozwa na mkuu wa kituo cha utamaduni na habari za kimataifa katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Jassaam Saidi, akawaeleza wageni kuhusu miradi ya Ataba pamoja na kuwaonyesha filamu mbili zinazo onyesha bidhaa zinazo tengenezwa na Atabatu Abbasiyya, kisha akakaribisha maswali na maoni kutoka kwa wageni, alijibu maswali yote aliyo ulizwa”.

Mazungumzo yakafungwa kwa kusema: “Hakika ziara zetu zitaendelea kwa kuwasiliana na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, hakika miradi ya Ataba ni mizuri inafaa kupongezwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: