Ratiba ya (zawadi ya mfungaji)… kujibu maswali yanayo husu mwezi wa Ramadhani.

Maoni katika picha
Majibu mazuri yanatolewa katika ratiba ya (zawadi ya mfungaji) inayo fanywa kila siku ndani ya mwezi wa Ramadhani kwenye ukurasa wa video wa mtandao wa kimataifa Alkafeel, na kwenye chanel ya kituo cha uzalishai Alkafeel katika youtube pamoja na baadhi ya vyombo vya habari.

Program hiyo imetengenezwa na kituo cha uzalishaji Alkafeel kwa kushirikiana na kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya, muda wa video moja ni kati ya dakika tatu hadi tano, kunakua na maswali tofauti ya Dini yanayo husiana na hukumu za funga.

Program hiyo inaendeshwa na Sayyid Muhammad Mussawi kutoka kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya, anafafanua mambo muhimu anayo weza kukutana nayo mfungaji katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, unatolewa ufafanuzi kwa upana, inakua rahisi kuelewa kila mtu.

Kumbuka kua program ya (zawadi ya mfungaji) imepata mwitikio mkubwa kutoka kwa waumini kutokana na mambo yaliyomo yanayo husu mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kuangalia program hiyo ingia katika linki ifuatayo: https://www.youtube.com/watch?v=ZfC6dpxH4Zc au kwenye youtube: https://www.youtube.com/watch?v=ZfC6dpxH4Zc
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: