Maagadi ya Quráni katika wilaya ya Hindiyya imesimamia zaidi ya vituo (28) vya usomaji wa Qur,ani katika mwezi wa Ramadhani.

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya mwezi wa Ramadhani iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ni utaratibu wa matawi yake kusimamia vikao vya usomaji wa Quráni, hivyo tawi la wilaya ya Hindiyya katika mkoa mtukufu wa Karbala limefanikiwa kusimamia vikao vya usomaji wa Quráni zaidi ya (28).

Kiongozi wa Maahadi ya Quráni Shekh Jawadi Nasrawi amesema kua: Vikao vya usomaji wa Quráni ni ratiba maalum inayo tekelezwa na Maahadi katika siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani, inatokana na maelekezo ya Atabatu Abbasiyya tukufu yanayo lenga kueneza utamaduni wa usomaji wa Quráni katika jamii.

Kumbuka kua Maahadi ya Quráni inasimamia vikao vingi vya usomaji wa Quráni ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala kwa lengo la kusambaza utamaduni wa kusoma Quráni katika jamii, sambamba na kutengeneza kizazi kinacho fuata mafundisho ya vizito viwili Quráni na kizazi kitakasifu, Maahadi inaratiba maalum inayo tumia katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: