Ofisi ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeunda kamati itakayo simamia maonyesho inayo andaa.

Maoni katika picha
Ofisi ya wanawake chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya hivi karibuni imeunda kamati ya kusimamia maonyesho ya kielimu na kitamaduni, wanayo andaa na yale wanayo shiriki.

Kwa mujibu wa maelezo ya wasimamizi kamati hiyo ni kwa ajili ya kuboresha maendeleo katika shughuli wanazo fanya, ikiwa ni pamoja na kuandaa maonyesho au kushiriki katika maonyesho wanayo karibishwa.

Shughuli ya kwanza ya kamati hiyo ilikua ni kushiriki semina maalum chini ya usimamizi wa Ustadh Qatiba Azizi Hassan, kiongozi wa maonyesho katika kituo cha kutengeneza nakala kale na mkufunzi mkuu, amesema kua: “Semina hiyo inahusu mbinu za maonyesho, na kila kinacho husiana na maandalizi kamoja na mpangilio, wakina dada wamevutiwa sana na semina kutokana na aina ya maswali waliyo kua wanauliza, hawakutaka kupitwa na kitu chochote kikubwa au kidogo, wameonyesha umahiri wao katika sekta hii na uthubutu wa mwanamke”.

Bibi Aamali Kaadhim mmoja wa watumishi wa idara ya wanawake na mshiriki wa semina amesema kua: “Semina inahazina kubwa ya elimu na maarifa, ni muhimu sana kwetu kupewa semina za aina hii kwani zitatusaidia tuweze kutoa huduma bora”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: