Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanafanya kazi kubwa ya kuwahudumia mazuwaru watukufu katika mwezi huu wa Ramadhani, wanajitahidi kuwatengenezea mazingira mazuri, miongoni mwa kazi kubwa ni zile zinazo fanywa na idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi, idara hiyo kila siku inatandika mazulia katika eneo lote linazo zunguka haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ili kuwawezesha mazuwaru wengi zaidi kukaa karibu na kaburi la mnyweshaji wenye kiu Karbala wakati wa kufuturu, wanakunywa maji huku wanakumbuka kiu yake na ya ndugu yake Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake watukufu (a.s).
Pamoja na kuongezeka joto ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, lakini idara ya usafi katika kitengo cha utumishi imehakikisha inaweka mazingira mazuri kwa mazuwaru, eneo leto linalo zunguka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hutandikwa mazulia kwa vipande vipande, kuna sehemu maalum za kukaa wanafamilia na sehemu za kukaa kila mtu.
Kila sehemu huwekwa maji baridi ya kunywa pamoja na kuwepo mtumishi kwa ajili ya kuwapatia huduma mbalimbali watakazo hitaji, pamoja na kusafisha wakati wote au kutwaharisha sehemu itakayo patwa na najisi.
Baada ya mazuwaru kuongoka mazulia hayo hutanduliwa na kuwekwa katika stoo ya karibu kisha husafishwa sehemu hizo na kutandikwa mazulia mengine kwa ajili ya siku inayo fuata.
Fahamu kua kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya ni sawa na vitengo vingine, kinafanya kazi wakati wote mwaka mzima, na kazi zake huongezeka zaidi wakati wa matukio maalum.