Ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu imetaja kiwango cha Zakatul-Fitri ya mwaka huu.

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Hussein Sistani imesema kua kiwango cha Zakatul-Fitri mwaka huu ni dinari elfu moja na mia tano (1500) kwa mtu mmoja kama mbadala wa unga.

Kiwango cha Zakatul-Fitri ni pishi, sawa na kilo tatu za ngano, shairi, zabibu, mchele, tende au nafaka yeyote inayo pendwa zaidi na watu wa jamii husika, au utoe thamani ya pesa inayo lingana na nafaka hizo, ni wazi kua thamani yake inatofautiana kutokana na kutofautiana kwa nchi, kwa hiyo mtu anayetoa pesa yapasa ajue kiwango halisi cha bei ya nafaka hizo.

Fahamu kua pesa inayo tolewa katika Zakatul-Fitri sio sehemu ya zaka, kwa sababu Zakatul-Fitri sio ya kulipa pesa, bali pesa hizo ni mbadala wa pishi (kilo 3) za chakula, kwa hiyo mtu anapotoa pesa anatakiwa ajue kua pesa hiyo ni mbadala wa chakula.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: