Dokta Aqeel Alaa mkuu wa kitengo cha elimu katika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu amempokea mwenzake wa chuo kikuu cha Karbala Dokta Ahmadi Yasari, wakajadiliana mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushirikiano wa kielimu na kitafiti.
Mwisho wa mazungumzo yao Dokta Aqiil akasema: “Hakika chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya juhudi ya kuimarisha uhusiano na taasisi mbalimbali za elimu za serikali na binafsi, kwa ajili ya kubadilishana uzowefu na kufanya kazi kwa ushirikiano, tunaushirikiano mzuri na vyuo vikuu mbalimbali kikiwemo chuo hiki cha Karbala”.
Akaongeza kua: “Leo tumejadiliana na Dokta Ahmadi Yasari kuhusu kufanya semina ya pamoja kati ya taasisi hizi mbili, itakayo ongeza kiwango cha ujuzi wa watumishi wa vyuo, na kubadilishana uzowefu, chuo kikuu cha Al-Ameed kinatilia umuhimu mkubwa semina za kujengeana uwezo”.