Kwa bei zinazo endana na familia za wairaq: Bidhaa za chakula zinazo tengenezwa na Alkafeel zatoa ushindani mkubwa katika mwezi wa Ramadhani ulio shuhudia kupanda bei za bidhaa.

Maoni katika picha
Pamoja na kupanda bei za vitu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani lakini bidhaa zinazo tengenezwa na Alkafeel hazikupanda bei, pia iliongeza utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya familia za wairaq, bidhaa hizo zimesaidia sana katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Shirika la Nurul-Kafeel linalo zalisha bidhaa za nyama na vyakula liliongeza uzalishaji tofauti za zamani, na kufanikisha kutoa kapu lililojaa vyakula vya aina tofauti, halikuishia kutoa bidhaa kavu au za viwandani peke yake, bali limetoa hadi mazao ya shambani kwa kupitia mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s), kama vile nyanya, tango, pilipili, bilinganya na mengineyo, na bidhaa za nyama zilitoka kwenye zizi za mbuzi na ngómbe ambazo wanyama walichinjwa huko kisha nyama zikasambazwa katika vituo vya mauzo vilivyopo sehemu mbalimbali katika mji mtukufu wa Karbala.

Shirika likatoa tangazo kwa mtu yeyote atakae pandishiwa bei au akaona tatizo lolote kwenye vituo vyetu awasiliane moja kwa moja na ofisi ya mahusiano na ufuatiliaji kwa kutumia namba hizi (07801966624), au namba ya mauzo na masoko (07801966622), au atume barua pepe kwa anuani hii hq@islamicalkafeel.com.

Kumbuka kua shirika la Nurul-Kafeel linalo tengeneza bidhaa chini ya Atabatu Abbasiyya lilitangaza kua linabidhaa zaidi ya (200) ikiwa ni pamoja na nyama na pidhaa mbalimbali vya vyakula, shirika hili linafanya kazi chini ya muongozo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, limeazimia kusaidia uzalishaji wa ndani wa bidhaa bora kwa bei rahisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: